Korosho za wakulima zipatazo tani 68 katika vyama vya msingi vya Chemana na China, kata ya Chitekete Halmashauri ya wilaya Newala Mkoani Mtwara, zimerejeshwa kwa wakulima baada ya kukataliwa kuingizwa kwenye maghala makuu wilayani humo.

Mwenyekiti wa chama cha Msingi Chemana Abilahi Ibadi, amesema kuwa Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima ni tani 15.6, huku Mwenyekiti msaidizi wa chama cha Msingi China Juma Samli, akidai kuwa Korosho zilizorejeshwa kwa wakulima walio chini yake ni Tani 53.

Aidha, viongozi hao wa vyama vya msingi wamesema kuwa licha ya kufanyika kwa jitahada mbalimbali za kuzichagua na kuzianika ili zikubaliwe kuingizwa kwenye maghala makuu kuuzwa, lakini juhudi zao hizo zimegonga mwamba.

Wakizungumza kwa nyakati tofuati, wakulima wilayani Newala wamesema kuwa kusikitishwa na hali hiyo, kwani mategemeo yao yalikuwa ni Korosho hizo kuuzwa ili wajipatie kipato kitakachowawezesha kujikimu na kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kununua pembejeo za kilimo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

“Wahindi walikuwa wanasafisha korosho mpaka wanazitafuta na kumaliza zote, Korosho zetu siyo chafu ni nzuri, ukiziangalia ni kavu, hazina unyevunyevu lakini zimerudi, watunza maghala wanazikataa, hivi mkulima ana soko uko nyumbani!?”,  amesema Fakihi Ahmadi Mpwato, Mkulima wa Kijiji cha Chitekete.

 

Mwinyi Zahera kuibwagwa Yanga, sasa kurithi mikoba ya Hans van der Pluijm Azam FC
Video: Kiapo cha Chadema champeleka Mdee mahabusu, Familia zaweka 'msiba' waliofungwa maisha