Mshambuliaji Lionel Messi amekaidi amri ya kupumzika mazoezi kwa siku moja, baada ya kurejea mjini Barcelona akitokea nchini Argentina ambapo alikwenda kuitumikia timu yake ya taifa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa kusini mwa Amerika.

Messi alishauriwa kupumzika kwa siku ya jana, ili leo ajiunge na wenzake kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani siku ya jumamosi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Malaga.

Mchezaji huyo mashuhuri dunaini aliona amri hiyo kama mzigo kwake, na badala yake alijumuika na wachezaji wa kikosi cha pili, kitendo ambacho kiliheshimiwana benchi la ufundi la FC Barcelona.

Meneja wa FC Barcelona Luis Enrique, alisema walipanga kumpumzisha Messi kwa kuamini alikua amechoka kutokana na majukumu mazito yaliyomkabili kwa zaidi ya juma moja akiwa na timu yake ya taifa.

Alisema baada ya mchezaji huyo kuamua kufanya mazoezi na kikosi cha pili, kila mmoja aliheshimu maamuzi hayo, ambayo amekiri yalizusha hofu miongoni mwao kwani walishindwa kufuata ushauri uliokua umetolewa na wataalamu wa tiba.

Wachezaji wengine ambao walikua wamerejea mjini Barcelona wakitokea katika timu zao za taifa, walitii agizo la kupumzika kwa siku moja na leo wanaanza rasmi mazoezi.

Wachezaji hao ni Javier Mascherano, Sergio Busquets, Sergi Roberto, Denis Suarez, Marc-Andre ter Stegen pamoja na Lucas Digne.

Arsene Wenger Amkataa Mathieu Debuchy
FIFA Kuzichunguza England, Scotland