Aliyekua Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Luis Miquissone amesema ana matarajio makubwa ya kufanya vizuri zaidi akiwa na klabu yake mpya Al Ahly ya Misri.

Miquissone alijiunga na Al Ahly ya Misri mwezi Agosti akitokea Simba SC, baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwenye mchiuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu uliopita 2020/21.

Miquissone amesema, ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha wababe hao wa Misri kutokana na uzoefu mkubwa alioupata akiwa nchini Afrika Kusini na Simba SC.

“Kwangu ni jambo kubwa kujiunga na klabu kubwa kama Al Ahly, hii ni ndoto ya kila mchezaji mwenye malengo ya kuwa mchezaji mkubwa, hivyo ilikuwa furaha kwangu kucheza dhidi ya Al Ahly nikiwa na klabu ya Simba kwenye Ligi ya mabingwa Afrika msimu uliopita.”

“Nimejifunza mambo mengi nikiwa na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini lakini pia nikiwa na Simba kwa misimu miwili niliyokuwa Tanzania, naamini kuwa uzoefu nilioupata nikiwa Afrika Kusini na ndani ya Simba utanisaidia kufanya vizuri katika majukumu yangu nikiwa na Al Ahly.” amesema Miquissone aliyeitumikia Simba SC kwa misimu miwili 2019/20 na 2020/21.

Akiwa na kikosi cha Simba SC kwa misimu miwili iliyopita, Luis alifanikiwa kucheza michezo 37 ya Ligi Kuu Bara, na kuhusika katika mabao 25 akifunga mabao 12 na kuasisti mara 13.

Rivers United kujipima kwa Enyimba FC
Bilioni 165 kujenga uwanja wa Ndege Msalato