Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wamelaani mradi wa uelimishaji uliolenga katika kutoa elimu ya Virusi Vya Ukimwi ambao umeonekana kuwa na upande wa pili wa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja katika Manispaa hiyo.

Wakiongea hivi karibuni katika kikao cha madiwani wa Manispaa hiyo, madiwani hao walieleza kuwa  mradi huo unaendesha semina ambayo pamoja na mambo mengine inaelezea namna ya kutumia mafuta ya kulainisha wakati wa kujamiiana kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikidai kuwa ni njia ya kuwaepusha na uwezekano wa kupata maambukizi ya vizuri.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Lewis Kalinjuna alieleza kuwa hakuwa na taarifa yoyote ofisini kwake kuhusu mradi huo hivyo haukufuata utaratibu ingawa ulidaiwa kuratibiwa na baadhi ya viongozi.

“Sasa kama watendaji wanaalika watu bila barua ya Mkurugenzi, huoni hapo kuna tatizo. Kuna tatizo kubwa sana. Niombe watu wa Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mkurugenzi muanze mambo yenu kwa uchunguzi kuanzia kwa watendaji wa kata, wawaambie walinzaje kuwakubalia hawa watu na kuanza kuwaita watu kwenye semina ambayo inaudhi. Ni semina mbaya sana Mheshimiwa Mwenyekiti ina haharibu Jamii yetu,” alisema Diwani mmoja wa Manispaa hiyo.

Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu, Takukuru Waitiwa Ushahidi
Magufuli amemtumbua jibu Balozi Sefue kutokana na haya?