Sakata la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya ujenzi limechukua sura mpya.

Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.

Muitaliano huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.

Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa aina yoyote katika biashara yao.

“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.

Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake. Alisema baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika mzozo. Kwa mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio vinginevyo. Alisema kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu.

Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.

Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara hiyo na yuko tayari kuwakabidhi Takukuru.

Kwanini Mange amelivalia njuga suala hilo hata kama Muitaliano atamkana?  Ni dhahiri kuwa Mange amekuwa katika ugomvi na familia hiyo kwa muda mrefu hususan baada ya kumkamata na kumtupa Polisi Osterbay miaka iliyopita kwa kile kilichodaiwa kuwatolea lugha za matusi mtandaoni.

Yes it is indeed the biggest punishment ever. . . Jamani sina ushirikiano wa Muitaliano anymore Ila Muitaliano alishanipa enough to take them down anyways. . . Niko tayari kuwapa Takukuru email hii nzima waone Enzo alichomwandikia Mwamvita kuhusu January Makamba na kumtishia kuanika! Mpaka Mwamvita amjibu Hivi……In short it’s about January Accepting a huge amount of cash from Avery questionable character . . Sito publish hapa sabbau pia nitakuwa nawasidia wao ku over their tracks. Hata Kama wahusika wakidelete hizi email , serikali still ina uwezo wa kuomba records zooote za email hawa hawa wahusika wooooote. Hii email Ndo jamaa alikuwa anawatishia cha mwisho mwisho wampe pesa zake kabla hajaanika issue wakadhani anatania! Kesho yake ndo akaja kwangu. . . Ila dah binadamu wabaya sana, hamuwezi mkaamini mnajua Muitaliano Sasa Hivi eti ananiomba niache kuposti? Ananiambia niachane na issue And respect his decision. Imagine, now ananiomba niwaprotect Makambas especially January. Ananiambia kabisa leave January alone ??????… Yani ukisoma messages zake wakati kadhulimiwa alivyokuwa anatia huruma and now unaweza shangaa.. Eti just stop Na huna ruhusa ya ku publish vitu nilivyokutumia in private . Ila nime mjibu vizuri nime mwambia I’m glad nimekusaidia Sasa niache niwasaidie Watanzania. I swear next time kabla sijamsaidia Mtu nitawasainisha mikataba mpaka! But nilichoelewa Ni kwamba I think kawaambia Kuwa hakuna vitu vingine alivyonitumia Au alivyoniambia so Sasa wanavurugana. . . You guys know what? Hata Kama serikali ikiangalia pembeni but guess what 2020 is not far tunasubiria CCM watuambie eti January Makamba ndo mgombea wao waone Kama hatutompa nchi Halima Mdee!! ??????. . . Oh yeah just to add, ile Safari ya Dubai, hata Mwamvita pia alikuwepo. In short it’s a family affair. Ja Ja Ja Ja…. . . Basi immediately baada ya kumalizana Na Muitaliano Mwamvita akaenda kuweka caption eti NEXT?

A photo posted by @mangekimambi_ on

Unyama: Mwanafunzi abakwa na kuuawa kikatili
Madiwani wauwakia mradi unaohamasisha 'Ushoga' Shinyanga