Rais John Magufuli ameikacha safari ambayo ingekuwa ya kwanza kwake nje ya Afrika Mashariki tangu aingie madarakani, na kuamua kwenda jijini Kampala nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni.

Rais Magufuli alikuwa na ratiba ya kwenda jijini London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano unaouhusu mapambano dhidi ya rushwa, unaofanyika kesho. Rais Magufuli alikuwa kati ya marais wawili pekee Afrika walioalikwa, mwingine ni Muhammudu Buhari wa Nigeria.

Hata hivyo, Rais Magufuli amemtuma Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhudhuria mkutano huo muhimu kwa niaba yake akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga.

Waziri Mkuu alithibitisha jana jijini Dar es Salaam kuhusu safari hiyo ya Uingereza kumuwakilisha Rais Magufuli.

Majina ya vigogo 45 wenye akaunti nono nje yaanikwa
Makonda anasa Sukari, Aliyekutwa na tani kadhaa adai hugawa bure