Panga la Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. John Magufuli limeendelea kupunguza matumizi ya Serikali ambapo hivi sasa ametangaza kuwapunguzia mishahara watumishi waliokuwa wanalipwa mishahara minono ya mamilioni.

Akizungumza jana Mjini Chato Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema kuwa wamebaini kuwepo kwa wafanyakazi wa Serikali ambao wanapokea mshahara hadi shilingi milioni 40 kwa mwezi na kwamba ameazimia kuwapunguzia fungu hilo hadi shilingi milioni 15.

“Kuna baaadhi ya wafanyakazi nchi hii wanapata mishahara hadi milioni 40 kwa mwezi. Hakika nawaambia mishahara hiyo nitaifuta. Nataka mshahara wa juu uwe milioni 15. Nitaishusha ili iende kwa hao wadogo wanaoteseka. Kuna watu wanaishi kama malaika nataka niwashushe waishi kama shetani. Ambaye hawezi aende anakotaka,” alisema Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alisema kuwa katika zoezi la kupunguza wafanyakazi hewa, kwa muda mfupi tayari wameshabaini idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambao wataondolewa kwenye orodha ya malipo (payroll).

Alisema zoezi hilo limefanikisha kubaini uwepo wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ambaye hupokea mishahara 17 kupitia akaunti tofauti na kwamba Serikali imeamua kumfikisha mahakamani.

Baada ya Marekani Kuinyima Tanzania Msaada, Mashirika haya yajitokeza kusaidia
Uliiona hii Video? Raila Odinga aanguka na Jukwaa akisimulia ya 'Yesu na Shetani'