Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba SC Amos Makalla, ameupongeza Uongozi wa Klabu hiyo kwa kumpata Afisa Mtendaji Mkuu Mpya ‘CEO’ Imani Kajula.

Simba SC inafanya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa viongozi leo Jumapili (Januari 29) katika Ukumbi wa Mikitano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Makalla ametoa pongezi hizo alipokuwa akihutubia Mkutano huo baada ya kutambulishwa na kukaribishwa na Mwenyekiti Murtaza Mangungu.

“Hongereni sana Wanasimba, mmepata CEO mzuri, anafanana na aliyepita. Kajula ni mtu wa mpira. Lakini pia mmepata msemaji sahihi, anafanya kazi nzuri sana.”

“Naamini mmekuja kutimiza jukumu la kikatiba. Lakini niwapongeze kwa mafanikio iliyopata Simba.”

“Simba sasa kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni jambo la kawaida, hayo yote ni mafanikio, ifike mahali tuwe wakweli, tumtie nguvu mwekezaji Mohamed Dewji Mo”

“Najulikana ni Simba lakini sababu ya ukuu wangu wa mkoa inabidi kutendea haki na timu nyingine. Mimi ni Simba.”

“Tushindane kwa hoja lakini tukiitanguliza mbele Simba, Simba kwanza, mtu baadae.”

“Nilikutana na Mohamed Dewji ‘Mo’ wakati anasafiri akaniambia uwanja tutaujenga mjini nataka eneo lingine kubwa zaidi, tuweke academy, nataka kufanya mambo makubwa zaidi ya Simba, ameniambia mimi lakini mtandaoni unaona Mohammed kujionda Simba.” amesema Makalla.

Imani Kajula aweka wazi Simba SC inakoelekea
LATRA yakumbushwa weledi kazini, kuepuka rushwa