Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba, amesema kuwa kauli iliyotolewa na Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima, aliyedai kwamba chanjo ya Corona iliyoletwa nchini ina madhara kauli hiyo haikubaliki.

Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa ukurasa wake wa Twitter, mara baada ya uwepo wa video clip zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonesha mbunge wa Kawe akidai kuwa Tanzania ilikuwa imeshashinda Corona na kwamba chanjo ya Corona ni mpango wa mataifa ya nje kuwaangamiza Watanzania.

Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki, ni hatari kupotosha watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo, mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba serikali imeileta kuwadhuru watu si sahihi,” ameandika Makamba.

Tanzania ilipokea dozi zaidi ya milioni 1 za chanjo ya Corona kutoka Marekani kupitia mpango wa usambazaji chanjo ya Corona wa COVAX.

Rais Samia kuzindua chanjo kwa kuchanjwa
Masau Bwire amvaa Bernard Morrison