Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda au Baba Keagan leo ametimiza miaka 7 ya ndoa yake jambo ambalo amemshukuru Mungu kutokana na misukosuko aliyopitia na bado ndoa yake kuwa imesimama imara.

Kubwa kuliko yote amemshukuru Mungu kwa kumjalia furaha ya maisha yake ambayo ni mtoto aliyejaaliwa kumpata mapema mwaka huu.

”Siku ya leo nimetimiza miaka saba ya ndoa yangu, lakini nikitizama njia tuliyopita bado nawaza tumewezaje kufika na ndipo ninapomrudishia Mungu utukufu” ameandika Makonda.

Makonda amesema katika miaka yake saba ya ndoa amepitia vigingi vingi ametaja vikiwemo vya kuchafuliwa kwenye magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kutukanwa matusi ya kila aina.

Pia amemshukuru mke wake kusimama naye nyakati zake zote za shida na raha mpaka leo kufikia hapa walipofikia ikiwa ni pamoja na kutimiza miaka saba ya ndoa yao jambo ambalo sio wengi wamefanikiwa kulihimili.

Kupitia ukurasa wake wa Instgrama Makonda ameandika waraka mrefu uliozungumzia maisha yake hasa na familia yake na utukufu wa Mungu juu ya maisha yao.

 

Sadio Mane kurejea kikosini leo
Alli, Danny Rose, Vertonghen kuikosa PSV Eindhoven

Comments

comments