Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Najib Razak amekutwa na hatia katika mashtaka yote saba ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 pamoja na faini ya Dola Milioni 49 (takriban Tsh. Bilioni 113.9).

Hukumu yake imetolewa siku 6 baada ya Mahakama Kuu kuamuru ailipe Serikali Dola Milioni 400 ikiwa ni kodi na faini ambazo hazikulipwa kati ya mwaka 2011 hadi 2017.

Ufisadi huo unahusiana na kashfa ya mabilioni ya dola yaliyokuwa yametolewa na serikali kwa ajili ya mradi wa maendeleo.

Fedha za mradi huo ziliibiwa na kuelekezwa katika matumizi binafsi, yakiwemo ununuzi wa magari ya anasa na kazi za sanaa zenye gharama kubwa.

Hukumu hii dhidi ya Najib Razak ilichukuliwa kama kipimo kwa utawala wa sheria nchini Malaysia, kwani imetolewa miezi mitano tu baada ya muungano unaokijumuisha chama cha Razak kushinda uchaguzi, ambapo wengi walihofu kuwa ushindi huo ungeshawishi uamuzi wa mahakama.

Akitoa hukumu hiyo leo, jaji wa mahakama ya juu ya Malaysia amesema upande wa waendeshamashtaka umeweza kutetea hoja yake vyema na kuondoa mashaka yote juu ya hatia ya Razak.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la mahakama mjini Kuala Lumpur mchana wa Jumanne (29 Julai), Najib alisema kuwa mashitaka dhidi yake yalikuwa ya kisiasa na kwamba hahusiki na kadhiya hiyo ya ubadhirifu wa kiasi cha mabilioni ya dola yaliyotoweka kwenye mfuko wa maendeleo wa serikali, maarufu kama kashfa ya 1MDB:

Polisi walivyozuia ndoa ya mwanafunzi katavi
Wilaya Bukoba yapungukiwa madarasa 1,297 ya shule za msingi.