Baada ya sakata la muda mrefu la tuhuma za rushwa  linalomkabili Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, hatimaye Jaji Mkuu nchini Brazil ameagiza kushikiliwa kwa mali za Rais huyo baada ya kukutwa na hatia ya rushwa.

Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Sergio Moro amesema kuwa kiasi cha dola za Marekani laki mbili zimegunduliwa katika akaunti ya kiongozi huyo wa zamani, hivyo kupelekea kushikiliwa kwa mali anazomiliki yakiwemo maghorofa matatu , ardhi kubwa ambayo alijimilikisha na magari mawili ya kifahari.

Aidha, Rais huyo wa zamani aliyejipatia umaarufu wa kuwatumikia wananchi wake kwa kuweka sera ya kuwajali wanyonge, alitumia fursa hiyo kuweza kujitajirisha kwa kuiba mali za umma.

Hata hivyo, Da Lula ataendelea kuzitumia mali zake hizo endapo atashinda katika rufaa yake aliyoikata ya kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama nchini humo ya kwenda jela miaka tisa na nusu iliyotokana tuhuma za rushwa.

Rais huyo wa zamani wa Brazil, hivi karibuni alihukumiwa kwenda jela miaka tisa na nusu mara baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za rushwa ambazo zilikuwa zikimuandama.

LIVE: Ziara ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza nchini Tanzania
Video: Lissu agomea kortini..., JPM atangaza kiama kwa wauza mafuta