Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Lazaro Mambosasa amekanusha kutoa tamko la kuzuia wanawake kuvaa nguo fupi zisizo na heshima kwa maelezo kuwa suala la mavazi bado halijatungiwa sheria na swala hilo lipo kimaadili na si kisheria.

Amesema Jeshi la Polisi lina kazi ya kushughulikia makosa ya kisheria na si maadili.

Mambosasa ametoa kauli hiyo leo Januari 18, 2018 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Redio Clouds, ikiwa ni siku mbili baada ya kunukuriwa katika mkutano wake na wanahabari kuwa amezuia uvaaji wa nguo fupi na unyoaji wa aina ya kiduku jijini Dar es Salaam.

“Niliwaeleza wazi kuwa suala la mavazi bado halijatungiwa sheria hivyo polisi hatuhusiki nalo mtu anayevaa kimini katika maeneo kama kanisani au msikitini  ni ukiukwaji wa maadili,” amesema na kuongeza.

Aidha amesema kuwa suala la mavazi ni swala la kimaadili hivyo kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada zina jukumu la kushughulikia swala hilo lakini si polisi kama ambavyo taarifa imesambaa mitandaoni.

Amesisitiza, “Nilikwenda mbali zaidi na kuwaeleza kuwa hivyo vimini kuna mahali vinahitajika kama ufukweni, sehemu za starehe. Ikitokea mtu amepigwa, amedhalilishwa au amekamatwa na askari kwa kuwa amevaa kimini ana haki ya kulalamika kuwa ameshambuliwa.”

Simba yamtambulisha kocha mpya toka Ufaransa
Pierre Lechantre awasili, kuanza kazi haraka iwezekanavyo