Ilikuwa imepita miaka 65 tangu klabu ya Huddersfield Town ilipowafunga Manchester United lakini hapo jana iliwachukua dakika 5 tu kuichapa Man Utd ambayo ilikuwa haijapoteza mchezo katika mechi nane za ligi kuu ya EPL  msimu huu.

Manchester United wakicheza ugenini katika dimba la The John Smith’s Stadium, wamejikuta wakiambulia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa klabu ya Huddersfield ambayo imepanda daraja msimu huu.

Huddersfield walipata mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Aaron Mooy aliyefunga dakika ya 28 kabla ya Laurent Depoitre kupachika bao la pili dakika ya 33 na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Huddersfield kuwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kocha wa Man Utd Jose Mourinho alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Juan Mata na Anthony Matrial na kuwaingiza Henrikh Mhkitaryan na Marcus Rashford mabadiliko yaliyoifanya United kupata bao moja tu la kufutia machozi lililofungwa na Rashford dakika ya 78.

Kwa matokeo hayo Man Utd wameachwa jumla ya pointi tano na mahasimu wao Manchester City ambao wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley wakikusanya jumla ya pointi 25 wakati Man Utd wakiwa na pointi 20.

Mabao ya Manchester City yalifufungwa na Sergio Aguero dakika ya 30 Nicolas Otamendi dakika 73 na Leroy Sane aliyefunga bao la tatu dakika ya 75.

Man City 3-0 Burnley

Katika mchezo mwingine Chelsea wakicheza katika uwanja wo wa Stamford Bridge wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Watford, mabao ya Chelsea yakifungwa na Pedro Rodriguez, Michy Batshuay aliyefunga mabao 2 pamoja na Cesar Azpilicueta. Mabao ya Watford yamefungwa na Abdoulaye Doucoure na Roberto Pereyra.

 

 

 

Video: Mkakati wa kumng'oa Spika Ndugai wapikwa, Kitaeleweka
Mugabe aitikisa WHO, yafikiria upya uamuzi wake