Kiungo wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil ameripotiwa kuwaambia wachezaji wenzake kwamba atahamia katika klabu ya Manchester United pindi takapoondoka Arseanal.

Mkataba wa Ozil ndani ya klabu ya Arsenal unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kiungo huyo mjerumani hadi sasa hajasaini mkataba mpya huku kocha Arsene Wenger akikiri kuwa huenda akamuuza mwezi Januari ili asiondoke bure mwishoni mwa msimu.

Ozil anataka kulipwa mshahara wa £350,000 kwa wiki koasi ambacho Arsenal wamesema hawana na kutaka kumpa £275,000 pesa ambayo Mesut Ozil na wawakilishi wake wameikataa.

Kwa hali ilivyo ni wazi kwamba dirisha lijalo la usajili Mesut Ozil pamoja na Alexis Sanchez wanaweza kuondoka bure katika klabu hiyo kwani wote wawili mikataba yao inafikia ukingoni.

Manchester United wanafuatilia mienendo ya suala la Ozil na Sanchez kwa ukaribu na sasa inasemekana United wako katika nafasi nzuri kumchukua Ozil katiak dirisha la usajili mwezi Januari.

Ozil ana uhusiano mzuri sana na kocha wa United Jose Mourinho na walishawahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Real Mdrid jambo ambalo linaonekana linaweza kumvuta Mesut Ozil akakipige Old Traford.

Afisa wa tume ya uchaguzi Kenya IEBC ajiengua
Video: Lissu awaibua Nape, Ridhiwani, Wamebana wameachia