Mashetani wekundu (Manchester United) wamewasilisha ofa ya Pauni milioni 60 kwenye klabu ya Juventus, kwa lengo la kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa, Paul Pogba.

Man Utd wamewasilisha ofa hiyo itakayovunja rekodi ya usajili wa wachezaji waliowahi kujiunga na klabu za nchini England, endapo itakubaliwa na viongozi wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la The Sun, na taarifa zake kuchapishwa mapema hii leo, umoenyesha tayari ofa hiyo imeshatumwa na kwa sasa viongozi wa Man Utd wanasubiri jibu kutoka Juventus Stadium huko mjini Turin nchini Italia.

Uchunguzi huo umebaini kuwa, mpango huo wa Man Utd, umefanywa mapema kwa makusudi ya kutaka kuwapiku mabingwa wa soka nchini Hispania, FC Barcelona ambao pia wanamuwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.

Pogba celebrates a goal for United in the FA Youth CupPoul Pogba alipokuwa Man Utd

Meneja mpya wa Man Utd, wamedhamiria kumerejesha Pogba Old Trafford, ambapo ndipo alipokuzwa na kuendelezwa kipaji chake cha soka, baada ya kusajiliwa mwaka 2009, na kisha aliamua kuondoka mwaka 2012.

Katika ofa iliyotumwa kwa ajili ya usajili wa Pogba, mchanganuo wake umeonekana kuwa Pauni milioni 48 ni kama ada ya usajili na Pauni milion 12 italipwa baadae endapo kiungo huyo atafanikisha baadhi ya matarajio ya Man Utd ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji.

Rekodi ya usajili wa pesa nyingi katika klabu zinzoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, inashikiliwa na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Argentina Angel Di Maria ambaye alisajiliwa na Man Utd mwaka 2014, kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 59.7, akitokea Real Madrid.

Abdallah Ahmed Bin Kleb Awatosa Kiaina Kina Manji
Shiza Kichuya Athibitisha Kuihama Mtibwa Sugar