Kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya, amefunguka kuwa kama asingekuwa kambini na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, basi dili lake na kutua Simba lingekuwa limeshakamilika.

Kichuya anayetajwa kusaini mkataba wa awali na Simba kwa sasa yupo katika kambi ya Taifa Stars ambayo inayojiandaa na mchezo dhidi ya Misri kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ukiwa wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Kichuya amesema, tayari amefanikiwa kumalizana na Simba kwa ajili ya kujiunga nao kwa msimu ujao ambapo kwa sasa mchakato huo umeweza kusitishwa kutokana na yeye kuwepo katika kikosi cha timu ya taifa.

“Nimezungumza na Simba, kila kitu kimeenda sawa lakini kwa sasa mchakato umesimama mpaka pale nitakapomaliza majukumu ya timu ya taifa baada ya kucheza na Misri.

“Lakini nimewaambia kwa kuwa mkataba wangu na Mtibwa umebaki mwaka mmoja hivyo ni lazima wakazungumze na mwajiri wangu kwanza na wakikubaliana tu natua Simba na sitakua na sababu ya kukataa,” alisema Kichuya.

 

Manchester United Kuvunja Rekodi Yao Wenyewe Kwa Pogba
Mwakyembe ataka wabunge wa upinzani wasilipwe Posho