Ripoti ya uchunguzi uliofayika kwa miaka miwili imeeleza kuwa zaidi ya watoto 1,000 walidhalilishwa kingono na mapadiri katika jimbo la Pennsylivania nchini Marekani.

Akitangaza ripoti ya uchunguzi huo Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Pennsylivania, Josh Shapiro amesema kuwa maafisa wa Kanisa Katoliki wanadaiwa kuwapuuza wahanga wa udhalilishaji huo wa kingono na kuwalinda watuhumiwa wa vitendo hivyo.

Aidha, katika uchunguzi wao, jopo la wazee  wa mahakama liliwahoji mashahidi kadhaa na kufanikiwa kufichua zaidi ya nusu milioni ya kurasa za nyaraka kadhaa za siri katika Dayosisi nne tofauti nchini humo.

Hata hivyo, Nyaraka hizo za siri zinahusisha maelezo yaliyoandikwa na baadhi ya mapadri wakikiri kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji.

Miralem Pjanic kusaini mkataba mpya
Fred Lowassa ajiondoa ubunge Monduli, kisa chawekwa wazi