Klabu ya Everton iko mbioni kumtangaza kocha wa zamani wa Watford Marco Silva kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Sam Allardyce mwishoni mwa msimu.

Kocha huyo raia wa Ureno amekua chaguo la kwanza kwa mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri na anatarajiwa kupewa mkataba wa miaka mitatu ambao unaweza kuongezwa baadhi ya vipengele kutokana na mafanikio atakayoipa Everton.

Licha yakutimuliwa katika klabu ya Watford mwezi Januari baada ya timu hiyo kufanya vibaya Silva anatajwa kuwa mmoja wa makocha wanaofundisha aina ya mpira wa kuvutia na anatarajiwa kuleta upinzani kwenye ligi akitua Everton.

Everton ilifanya usajili wa wachezaji wengi akiwemo Wayne Rooney kutoka Manchester United lakini wamemaliza msimu katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu jambo lililopelekea kutimuliwa kwa Sam Allardyce.

 

Wabunge waruhusu wananchi kumiliki silaha Rwanda
Thiago Silva: Hatuahidi ubingwa, tunaahidi soka la ushindani

Comments

comments