Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi leo Septemba 23,2021 amekutana na maafisa wakuu waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dodoma, akiwemo IGP Simon Sirro ikiwa ni maandalizi ya kikao kati ya wadau wa siasa, msajili na polisi kitakachofanyika Oktoba 21, 2021.

Aidha mnamo Septemba 6, 2021, Jaji Mutungi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi imepanga kukutana na wadau wa siasa kufuatia malalamiko ya kutopewa fursa ya kufanya kazi zao za siasa kwa kuzuia kufanya makongamano mbalimbali.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema ipo sababu ya Jeshi hilo kuwa na ukaribu na viongozi wa vyama vya siasa sababu viongozi hao ni wadau muhimu katika masuala ya usalama na kusisitiza kuwa kwenye mikutano ya kisiasa ya ndani na ya nje wao wanachokizingatia ni usalama.

ukuaji sekta ya viwanda kutokomeza umasikini
Marekani kutoa chanjo ya ziada kwa wazee