Simba, Jackson Mayanja amesema hana matatizo na mchezaji hata mmoja na Simba, na hajawahi kugombana na yeyote kati yao.

Na kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Uganda, amesema kwamba haiwezi kutokea siku akagombana na mchezaji, ila anasikitika sasa kumeibuka kama kampeni ya kumchafulia jina lake kutokana na mafanikio aliyoyapa katika klabu hiyo.

Mayanja amesema kwamba amesikitishwa na sakata jipya lililoibuka kuhusu mshambuliaji Mganda mwenzake, Hamisi Kiiza.

“Nashangaa kuambiwa nimemfukuza Kiiza, mimi sijafanya hivyo, Kiiza alikuwa anawasiliana na Meneja tu (Abbas Ally) na tatizo lao lilikuwa katika kuvaa sare za timu wakati wa kwenda uwanjani na kupanda basi la timu,”amesema Mayanja.

Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar, amesema kwamba Meneja Abbas ametoa agizo la kuzuia wachezaji kwenda na gari zao binafsi kambini na pia wachezaji wote kutakiwa kuvaa sare wakati wa misafara ya kitimu.

“Sasa inapotokea mchezaji akakiuka maagizo ya Meneja, ni yeye ndiye anayeshughulikia, siyo mimi, mimi nawasubiri wachezaji uwanjani na Kiiza japokuwa alichelewa kurejea kutoka Uganda, wote yeye na Juuko (Murshid) niliwapokea mazoezini na nimeendelea kuwa nao,”amesema Mayanja.

Kiungo huyo wa zamani wa SC Villa na KCCA za Uganda amesema kwamba, matatizo yaliyojitokeza kati ya Meneja Abbas na Kiiza yamekwisha na mchezaji huyo yupo kambini Ndege Beach, Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa dhidi ya Coastal Union Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mayanja amesema hata matukio ya awali kuhusu wachezaji Hassan Isihaka na Abdi Banda pia yanapotoshwa, lakini ukweli ni kwamba hakuwahi kugombana na wachezaji hao.

“Ndiyo maana Isihaka baadaye alikuja kuniomba msamaha na leo amemaliza adhabu yake na tupo naye tena kwenye timu, lakini Banda hakuwahi kuja kuniomba msamaha hadi sasa na hajaja tena mazoezini,”amesema.

Aidha, Mayanja amesema hali ya kambi ya Simba ni shwari kabisa kuelekea mchezo wa wa Robo Fainali ya Kombe ka TFF dhidi ya Coastal Union na matarajio ni ushindi.

Habari Mpasuko: MAGUFULI AMNG'OA UKUU WA MKOA ANNE KILANGO
Mama Kanumba alia Lulu kumtupa, aomba 'japo salaam'