Mama mzazi wa muigizaji, marehemu Steven Kanumba amemlilia muigizaji aliyekuwa mchumba wa mwanae, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kwa kumsahau licha ya mengi yaliyotokea kati yao.

Akiongea na Clouds TV, Mama Kanumba alieleza kwa uchungu kuwa hakuna msaada wowote anaupata hivi sasa kutoka kwa mshindi huyo wa tuzo ya Africa Magic Viewers Choice Awards ikiwa ni pamoja na Salaam.

“Lulu hanisaidii kitu chochote na hata sura yake nimeisahau. Mimi sihitaji msaada, hata salaam tu inanitosha,” Mama Kanumba anakaririwa.

Siku chache baada ya kutoka rumande alipokuwa akikabiliwa na mashtaka ya kumuua Kanumba bila kukusudia, Lulu alimtaza Mama Kanumba kuwa mama yake na wawili hao walionekana kuwa na furaha pamoja huku wakitiana moyo kutokana na matatizo yaliyowafika.

Mayanja: Sijamfukuza Kambini Hamisi Kiiza
Mkataba Wa Neymar Wanaswa, Malipo Yake Yaanikwa Hadharani