Beki wa pembeni wa Chelsea Branislav Ivanovic huenda akatimka klabuni hapo mwanzoni mwa mwaka 2017, kupitia dirisha dogo la usajili.

Klabu ya Juventus inatajwa kuhusika na mpango wa usajili wa beki huyo ambaye amedumu Stamford Bridge tangu mwaka 2008, na tayari ameshacheza michezo 257 na kufunga mabao 22.

Sababu kubwa ya Juventus kumtazama kwa jicho la tatu beki huyo kutoka nchini Serbia, ni kutokana na hitaji walilonalo kwa sasa, la kumsaka mbadala wa Dani Alves ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Alves aliumia mguu mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Italia dhidi ya Genoa.

Hata hivyo Juventus wamejizatiti kuziba nafasi ya beki wa kulia kwa kuangalia wachezaji wengine endapo watamkosa Ivanovic, ambapo katika orodha yao imeripotiwa kuna jina la beki wa Manchester United Matteo Darmian pamoja na Mattia De Sciglio wa AC Milan.

Simbachawene apigilia msumali maadhimisho ya walemavu
Mathieu Debuchy Asukiwa Mipango Ufaransa