Mlinzi wa kati Rajab  Zahir aliyekuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Stand United akitokea  Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam  amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc  leo.

Kwenye ofisi za City zilizopo Mkapa Hall, eneo la Soko Matolla, jijini hapa, Zahir, amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kujunga na  kikosi cha kocha Kinnah phiri  na kusema kuwa ana imani kubwa ya kupata mafanikio yake  kisoka akiwa na chini ya kocha  huyo  bora  kutoka Malawi.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujiunga na City, hii ni moja kati ya timu kubwa nchini kwa sababu ina ushawishi wa kutosha  kwenye soka la nchini yetu, kitu muhimu ni kuomba ushirikiano kutoka kwa pande zote  kwa maana ya uongozi wachezaji wenzangu na mashabiki,  hayo yote  yatatufanya kutimiza malengo kwa sababu  kila mmoja anahitaji mafanikio katika kazi  kwangu mimi hapa ndiyo sehemu  ambayo nitayapata” alisema.

Zahir amejiunga na City baada ya msimu mmoja wa mkopo kwa Stand  United ya  Shinyanga  uliohitimisha kandarasi yake ya miaka 3 na kikosi cha  Yanga ya Dar es Salaam,

Akiwa Stand United, Zahir alifanikiwa kucheza michezo 23 katika mechi zote 30 zilizochezwa na timu hiyo ya Shinyanga na kufanikiwa kushika nafasi ya 7 ikikusanya jumla ya pointi 40 mwisho wa msimu  uliopita.

Meneja Kabla ya Kufuatilia Kazi Msanii unatakiwa Kujituma Zaidi- Petitiman Wakuache
UEFA Yataja Wanaowania Tuzo Msimu Wa 2015-16