Kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) imemfuta uanachama kada mkongwe wa chama hicho Bernard Membe kuanzia leo februali 28, 2020.

Akisoma taarifa katibu wa itikadi na uenezi, Humphrey Polepole, baada ya kikao cha kamatikuu kilichofanyika ofisi ndogo ya chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam, chini ya Mwenyekiti wa chama hicho dkt. John Magufuli, amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kupata adhabu mbalimbali ambazo hazijamsaidia kujirekebisha.

“Kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa imeadhimia kwa pamoja afukuzwa uanachama, uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonesha kuwa mwenendo waka toka mwaka 2014, amewahi kupata adhabu nyingine, zingeweza kumsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo” Amesema Polepole.

Kwa upande wa aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Omari Kinana, amepewa adhabu wa kalipio kutokana na kanuni ambayo inampa adhabu mwanachama aliyekipaka tope chama hicho.

Akisoma adhabu hiyo polepole amesema mwanachama akipata adhabu hiyo hatakuwa na haki ya kugombea nafasi yoyote lakini atakuwa huru kuchagua viongozi.

” Kamati kuu imepokea maelezo ya Abdulhaman kinana katibu mkuu mstaafu wa ccm, na imeadhimia apewe adhabu ya kalipio kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili toleo la 2017″ amesema Polepole.

Kada wa tatu wa CCM ambaye hukumu yake imetolewa na kamati kuu ni Yusuph Makamba ambaye amesamehewa baada ya kuomba msamaha kwa barua na kuonesha unyenyekevu.

“Kamati kuu imetoa msamaha huu kwa msingi kwamba mzee Makamba wakati wote tangu aliposomewa mashtaka yake amekuwa muungwana, mnyenyekevu na mtii kwa chama” Amesema Polepole.

Ikumbukwe kuwa vigogo hao walihojiwa na kamati ndogo ya maadili chini ya makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula baada ya sauti zao kusambaa katika mitandao ya kijamii wakieleza jinsi CCM ilivyopoteza mvuto na jinsi chama kilivyoshindwa kuwalinda makatibu hao dhidi ya mwanaharakati ambaye alikuwa akitoa tuhuma dhidi yao.

Sauti hizo zilianza kusambaa mitandaoni baada ya kinana na Makamba kuandika waraka Julai mwaka jana kwenda kwa katibu wa baraza la wazee CCM, Pius Msekwa wakidai uongozi hauwalindi dhidi ya mtu huyo ambaye walidai anawadhalilisha na huenda alikuwa analindwa na mtu mwenye mamlaka.

Aubameyang asikitika Arsenal kung'olewa Europa League
Serikali yaagiza ardhi ya kilimo itengwe kwa vijana

Comments

comments