Uingereza imesema kuwa itawafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi baada ya Moscow kukataa kutoa maelezo ya matumizi ya sumu ilivyokuwa ikitumika wakati wa utawala wa Soviet katika mji wa Salisbury- Uingereza kumshambulia jasusi wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal na binti yake, Yulia.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kuwa hatua hiyo inapelekea kuanza kwa vita ya kiuchumi dhidi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin na kikundi cha watu wachache wenye maslahi ya pamoja cha maafisa wa serikali ya Kremlin na wafanyabiashara matajiri wenye ushawishi wa kisiasa.

Amesema kuwa vikwazo hivyo vya kuwafukuza ni pamoja na kuzuia rasilmali zao ambazo wanazimiliki Uingereza pamoja na kunyimwa viza kwa watu binafsi wote waliotajwa katika sakata hilo.

Aidha, May amewashinikiza washirika wake wa Kimataifa kufuata hatua iliyochukuliwa na Uingereza na kuanza kuangaza mabilioni ya dola ambazo Kremlin imewekeza katika rasilimali zake ulimwenguni kote.

“Kwa jumla kile ambacho tumepanga kufanya kitakuwa na athari mbaya sana kwa Urusi, lakini ibadi iwe hivyo,”amesema afisa mmoja wa ngazi ya juu ya Marekani

Hata hivyo, mpango uliowekwa na Uingereza unakusudia kutaifisha, rasilimali na mali zote za Warusi iwapo hawatoweza kuonyesha chanzo cha mali na rasilimali zao zimepatikana kwa njia halali.

Prof. Tibaijuka awachana viongozi wa serikali ya awamu ya tano
Serikali yalivalia njuga tatizo la nguvu za kiume