Naibu Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,vijana na watu wenye ulemavu, AbdallaH PosSi leo amezindua mradi wa  Taasisi ya Great Hope inayotoa huduma ya kuwawezesha wanafunzi fursa ya kuvionyesha vipaji vyao pindi wanapokuwa shule ili waweze kujiajri pindi watakapomaliza shule.

Katika uzinduzi huo uliofanyika leo shule ya Sekondari Makongo Ukiunganisha shule mbalimbali ndani ya jiji la Dar es salaam  amesema kuwa mradi wa Great hope foundation uliopewa jina la Tuzo za Uwezo unaenda sambamba na malengo ya serikali ya kuandaa vijana watakao kuwa nguvu kazi ya Taifa.

DSC_0146

Aidha amewataka vijana kuwa wabunifu kwa kuandaa mipango ya kujiajiri pindi wanapokuwa wanahitimu masomo na kuondokana na dhana ya kuajiriwa huku akiwasisitiza elimu wanayoipata kutoka shule iwasaidie ktika kujitambua na kuendeleza uwezo nau vipaji walivyonavyo.

”kwa sasa Taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya vijana kutegemea kujiajiri jambo analodai limechangiwa na vijana wenyewe kuwa waoga wakutuhubutu kujiajiri”.Alisema Mh. Possi

Hata hivyo Mh. Possi amewataka wadau na taasisi mbali mbali kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika miradi tofauti tofauti ili kuwajengea vijana hao uwezo wa kujitambua na kujiamini kwamba wanaweza kufanya kazi kama watu wengine pasipo kubaguliwa.

Pamoja na hayo Possi, ameipongeza taasisi hiyo kuanzisha mpango huo ambao amedai utaweza kuwasaidia vijana katika kujikwamua kimaisha, kujenga mazingira ya kukabiliana na changamoto,stadi za uongozi,

Kwa Upande wake Mratibu wa Taasisi ya Great Hope,Noelle Mahuvi amesema nia iliyomugusa kunzisha ni baada ya kushuhudia mazingira magumu ya wanafunzi pindi wanapomaliza shule baada ya kukosa ajira huku akieleza kuwa  mpango aliounzisha utaanza katika shule kadhaa jijini dar es Salaam kwa lengo la kuwapa ujuzi wanafunzi wenye vipaji waweze kutimiza malengo yao.

DSC_0080

Bi Noelle ameongeza kuwa mradi huo umejikita hasa katika kuwafanya vijana waikumbuke jamii inayowazunguka kwa kuhakikisha kwamba miradi itakayokuwa inabuniwa na wanafunzi  hao italenga kuisaidia jamii kwa jinsi itakavyokuwa inawaingizia kipato.

 

 

Majani auona mwanga wa muziki wa Tanzania kwenye charts za Billboard
Magufuli amruhusu Mbowe kufanya maandamano Hai