Wizara ya Elimu nchini Tanzania imesema mitihani ya Kidato cha Sita iliyopangwa kuanza Mei 04 mwaka huu imehairishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini .

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Akwilapo amesema hilo wakati akizungumza na wazazi waliotaka kufahamu hatma ya Wanafunzi baada ya shule kufungwa tangu Machi kwasababu ya mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 .

Dk Akwilapo Amesema, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesambaza barua kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya zote pamoja na Shuleni ili kuwataarifu wanafunzi kuhusu kusitishwa kwa mitihani hiyo.

Ikumbukwe mnamo mwezi Machi mwaka huu waziri mkuu alitangaza kufungwa shule zote kuanzia awali mpka kidato cha sita kwa muda wa siku 30 na baadae kuongeza muda wa shule kufungwa mpka pale serikali itakapotoa tamko.

Hata hivyo, Wizara imewataka Wanafunzi kuendelea kujisomea wakiwa nyumbani.

Zimbabwe yatangaza punguzo la bidhaa kukabili corona
Mwakyembe: Roma hajatoroka nchini, corona imemkwamisha