Rais wa Marekani, Donald Trump ameagiza kuondolewa ulinzi kwa aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA John Brennan, akidai kuwa ni mtu asiyetabirika katika uadilifu na asiyefuata misingi.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Brennan amesema kuwa hatua hiyo ya Trump kumuondolea ulinzi ni mwendelezo wa jitihada za Rais huyo kudidimiza uhuru wa kujieleza na kuwaandama wakosoaji wa utawala wake.

Amesema kuwa jambo hilo linalopaswa kutiliwa mashaka na raia wote wa Marekani kuhusiana na mwenendo wa rais,na kuwatahadharisha pia wataalamu na wana usalama kuwa makini na hatua hizi za Trump.

Aidha, hivi karibuni Brennan alikaririwa akikosoa mkutano wa Trump wa mwezi July na rais wa Urusi Vladimir Putin uliofanyika mjini Helsinki kwamba haukuwa na maana yoyote.

Hata hivyo, kwa upande wake Donald Trump amepuuza madai hayo na kusema kuwa ni jambo linalozushwa tu kwa maslahi ya kisiasa.

Mkurugenzi ATCL akanusha Ndege ya Dreamliner kuwa na hitilafu
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 16, 2018