Mkoani Katavi wameshauriwa kuanzisha bucha maalumu kwa ajili ya kuuza nyama za viboko ikiwa ni mkakati wa kupunguza viboko waliopo katika bwawa la Milala ambao wamekuwa ni tishio kwa maisha ya wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Ushauri huo umetolewa na mhifadhi wa ujirani mwema wa hifadhi ya Taifa ya Katavi, Francis Kona kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya ya Mpanda (DCC) , awali kabla ya kutoa ushauri huo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo Meya Willy Mbogo waliomba wizara ya Maliasili na Utalii kuwaondoa viboko walio ongezeka kwenye bwawa la Milala.

Suala la kuwaondoa viboko hao lilijibiwa na mhifadhi aliye eleza kuwa ni suala gumu kuwahamisha viboko waliopo kwenye bwawa hilo na kuwapeleka kwenye hifadhi ya Taifa ya katavi kwani wanaweza kupoteza maisha kwa kupigwa na viboko watakao wakuta kwakuwa viboko huishi kwa ukoo na hawachangamani na ukoo mwingine.

Hivyo suluhisho ni kuandika barua ya kuomba kibali cha kuwauwa Viboko hao kisha kuanzisha bucha kwaajili ya kuuza nyama zitakazo kuwa zimetokana na viboko hao kwa wananchi kwaajili ya kitoweo kwa bei ya shilingi 1000 kwa kilo, pia itakuwa chanzo cha mapato cha halimashauri hiyo.

Aidha, Afisa Ardhi na Maliasili Halmashauri ya Nsimbo, Osephina Rupia amewaasa wananchi kujua jinsi ya kuishi na viboko vizuri ili wasiwajeruhi kwa kuacha kuwashabikia na kuwapigia kelele wanapo kuwa nchi kavu kwani huwasababishia hasira ambazo huwapelekea kuwajeruhi.

Treni yapata ajali jijini Dar
Kocha Scaloni amkumbuka Erik Lamela

Comments

comments