Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa viongozi wa vyuo hapa nchini kuchukulia kwa umuhimu jukumu la kuandika na kuielezea vema Tanzania katika vitabu kwa maslahi ya taifa.

Dkt. Mpango, ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waandishi pamoja na Wadhamini wa Kitabu cha “Continuity with vision – The Roadmap to success for President Samia Suluhu Hassan” wakiongozwa na Mhariri Mkuu wa Kitabu hicho, Prof. Ted Maliyamkono yaliofanyika hii leo Januari 28, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi pamoja naWadhamini wa Kitabu cha “Continuity with vision – The Roadmap to success for President Samia Suluhu Hassan” mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2023.

Amesema, ni vema kuendelea kuwapa moyo wasomi wa nchi hii ili kutambua kwambawanao wajibu wa kufanya tafiti na kuandika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisayansi katika taifa letu.

Aidha, Makamu wa Rais pia amewaasa watanzania kuendelea kujenga tabia ya kusoma vitabu pamoja na kuandika mazuri ya Tanzania kuanzia ngazi ya chiniili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwa kuandikwa na watu wa mataifa mengine.

Rais Samia azungumza na Mkurugenzi Kampuni ya mafuta UAE
Mahakama: Hakuna nusu kwa nusu ikivunjika ndoa