Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imesema kuwa hakuna Polisi yeyote wa kikosi hicho anayelipwa bonasi kutokana na ukamataji na ulipaji wa faini zinazotokana na makosa ya usalama barabarani.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kuwa hakuna trafiki yeyote anayepata bonasi kwa kukamata makosa.

“Nafikiri hii inatokana na kukamata makosa mengi,lakini niseme hakuna askari anayelipwa bonasi,wanachokifanya ni kukamata kulingana na makosa tu,”amesema Kamanda Mpinga.

Aidha, amesema kuwa zipo taarifa kuwa askari hao wamepangiwa idadi ya makosa, jambo ambalo sio kweli ila wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi kadri inavyowezekana, ikiwa ni kwa lengo la kudhibiti ajali.

 

Trump kuifuta sheria ya afya Obamacare
Kanisa lamuombea Rais Magufuli