Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani. 

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kitendawili’, aliondoka nchini Tanzania siku ya Jumatatu akiwa ameambatana na kikundi chache cha ngoma kikiwa na jumla ya watu sita pamoja na yeye mwenyewe.

Akiongea na mwandishi wetu akiwa nchini humo baada ya kuwasili katika eneo ambalo litafanyika tamasha hilo, Mpoto amesema Alhamisi hii wataanza kufanya maonyesha hayo katika tamasho hilo ambalo linayakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

Kama nilivyowaambia watanzania wakati naondoka Tanzania, tumekuja China kwaajili ya watanzania, tumekuja kuwawakilisha wao, tunatangaza utalii wa ndani, lugha zetu za makabila zaidi ya 120, lugha yetu hadhimu ya Kiswahili, mbuga zetu za wanyama kwahiyo sisi tutawaambia Tanzania ni nchi ambayo ina kila kitu kama ukiamua kuitembelea,” alisema Mpoto.

Muimbaji huyo amesema kila mtanzania anaweza kuitangaza nchini yake kwa mazuri hivyo wamewaka watanzania kuwa wazalendo na kudumisha amani iliyopo.

Mpina afunga machimbo ya mchanga wilayani Mkuranga
Hii ndio klabu anayokwenda Diego Costa