Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka Chadema kuacha kutumia tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kama ajenda katika kampeni za uchaguzi wa marudio na kusema kwamba chama hicho kimefilisika.

Ameyasema hayo akiwa Masasi katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM, ambapo amesema kuwa kitendo hicho cha Chadema kufanya kila mahali tukio hilo kama ajenda si kitendo kizuri.

“Mimi nitaenda kuwaambia wana Singida kwamba tuwaangalie vizuri hawa watu. Wao  ni mwenzao kwenye Chama sisi ni ndugu yetu na tunatoka sehemu moja. Inawezekanaje wawe wanafurahia tukio hilo? Kama kuna kitu walikuwa wanataka kitokee ili warushe maneno kwa serikali,”amesema Nchemba

Nchemba amesema kuwa Chadema wanamuona Lissu kama mtaji wa siasa ndiyo maana hata polisi walipomtaka dereva wake ili kuweza kumhoji waliamua kukaa naye huko.

Hata hivyo Nchemba amewataka wananchi hao kuichagua CCM kwa kazi nzuri inayofanya na kwamba kuuchagua upinzani wakitegemea itashinda ni sawa na kujeruhi nafsi zao

Kafulila aitosa Chadema
Saratani ya kibofu inamtafuna Eduardo Berizzo