Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC), Elisha Elia unatarajiwa kuzikwa kesho Jumanne October 27,2020 Mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa Baba Mzazi wa Marehemu Elisha, Mzee Elia Mwakagani mwili wa marehemu utapelekwa Kanisa la Kilutheri Segerea ambapo hadi saa 7 mchana itafanyika ibada ya kuaga mwili na kutoa heshima za mwisho.

Mara baada ya utoaji heshima za mwisho, safari ya kuelekea Mkoani Mbeya atakapozikwa Elisha itaanza.

“Msiba ulitokea juzi saa 10 jioni Hospitali ya Taifa Muhimbili na ratiba ya leo ni mwili kuwasili nyumbani saa 5 mpaka saa 6 mchana na utapelekwa Kanisa la Kilutheri Segerea ambapo hadi saa mchana itafanyika ibada ya kuaga mwili na kutoa heshima za mwisho na ikifika saa 8 mchana safari ya kuelekea Mbeya itaanza na mazishi ni Jumanne mchana” amesema Baba Mzazi wa Elisha.

Cioaba atoa neno kabla hajawavaa Mtibwa Sugar
Simba SC waahidi ushindi, mashabiki waitwa Uhuru