Mahakama Kuu ya Kenya imeamuru kurudishwa nchini humo kwa mwanasheria maarufu, Miguna Miguna ambaye alifukuzwa mara baada ya kumuapisha kiongozi wa NASA, Raila Odinga.

Jaji Luka Kimaru ameamuru Dkt. Miguna arudishwe Kenya kwa kuwa Serikali ilikaidi agizo la mahakama la kutakiwa kufikishwa mahakamani kwa mwanasheria huyo baada ya tukio la kumuapisha Raila Odinga.

Amesema kuwa hatua ya serikali kumfukuza Miguna ni kinyume cha katiba na sheria za kimataifa na kwamba mtu hawezi kupokonywa uraia wake.

Aidha, Miguna ni mzaliwa wa Nyando, Kaunti ya Kisumu lakini alipata uraia wa Canada alipoenda kusoma elimu ya juu na kuanza kufanya kazi za sheria.

Hata hivyo, kwa upande wa serikali imesema ilipaswa kumchukulia hatua kama hiyo Miguna baada ya kupata taarifa kutoka kwa usalama wa Taifa, kuwa mtu huyo ni hatari kwa usalama wa nchi.

 

Mkuu wa wilaya amshukuru mumewe kuongeza mke
Video: Kubenea amkalia kooni Mwigulu, ataka ajiuzulu