Mahakama jijini Conakry nchini Ghana imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, mwanamke mmoja aliyekutwa na hatia ya kuwadanganya wanawake wenzake kwa kuwapa dawa alizodai zitawafanya wawe wajawazito.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la N’na Fanta Camara, alikuwa akiwapa wanawake hao mchanganyiko wa madawa ya miti shamba yaliyofanya matumbo yao kuwa makubwa kama wajawazito, akiwataka kusubiri kujifungua.

Camara alikusanya pesa nyingi kutoka kwa wanawake zaidi ya 700 kama malipo ya tiba hiyo ili kuondokana na ugumba na kujipatia ujauzito kwa kutumia dawa za miti  shamba pekee.

Mbali na kifungo hicho cha miaka mitano jela, Mahakama pia ilimpiga faini ya $165,000 kama fidia kwa waathirika.

Hata hivyo, wanawake walioatapeliwa na madawa ya Camara wameeleza kutoridhishwa na adhabu aliyopewa, wakitaka apewe kifungo cha miaka mingi zaidi.

Watu wengine wawili waliounganishwa kwenye kesi hiyo pia kwa kumsaidia Camara, walihukumiwa vifungo vya miaka mitatu na miaka minne jela.

Kiwango cha mapato bandarini chapaa

Katika mashtaka yaliyowasilishwa, ilielezwa kuwa wanawake waliotumia dawa za Camara walipata wakati mgumu, wakiwa na dalili zote za ujauzito lakini hadi kipindi cha miezi 12 bado hawakuweza kujifungua.

Aidha, mwanamke huyo aliwakataza kwenda hospitalini kupima au kupata huduma yoyote kwa madai kuwa wataingilia matibabu yake, hali iliyowasababisha wengi kuendelea kusubiri bila mafanikio.

 

TALGWU yaishukuru Serikali, yampa tano Msukuma
Serikali kuimarisha hali ya usalama nchini