Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika  jimbo la Makunduchi Mkoa wa kusini unguja, kimekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.

Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe.Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni Makamu wa Rais wa JAmuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili kagtika kijiji hicho.

Akimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.

Aidha, amehaidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.

Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za maganda ya miwa na  makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.

Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi Day.

Waziri Wa Ujenzi Profesa Mbarawa Azindua Train Stesheni Mpaka Pugu
Hatua ya Kwanza Ya Usajili Azam FC wakamilika