Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa picha za darasa ambalo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zikimsumbua kiasi cha kuamua kuchukua jukumu la kufanya mabadiliko katika darasa hilo mpaka sasa kuwa shule.

Amesema kuwa baada ya yeye kuwa mbunge mwezi mmoja au miwili baadae zilianza kusambazwa picha za wanafunzi wakiwa wanasoma chini ya darasa hilo ambalo hali yake ilikuwa mbaya kwani lilikuwa ni darasa la miti tu huku wanafunzi wakikaa kwenye miti pia.

“Baada ya ile picha kuanza kusambaa mitandaoni, nilikuwa nasemwa mie, ndio maana nikaamua kuanza kuleta mifuko ya cement na kuanza kazi ya kufyatua tofali tukaanza na madarasa machache hivyo tulipigana kutoka kwenye hili darasa kwenda kwenye hayo madarasa mengine ambayo sasa yamefika manne na tunaendelea kwani tunataka iwe shule yenye madarasa ya kutosha na ikiwezekana na nyumba za walimu,”amesema Nape

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 5, 2018
Prof. Mbarawa anena kuhusu vichwa 11 vya Treni