Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameiomba Benki Kuu ya Dunia (WB), kuipa Tanzania mkopo wa Dola milioni 150, za Marekani ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma nchini.

Dkt. Mpango ametoa ombi hilo alipokutana na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam ambapo Waziri Mpango alifanikiwa kumuelezea Mkurugenzi huyo namna Uchumi wa Tanzania unavyokua.

Waziri Mpango ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania haswa hii iliyopo madarakani katika kutekeleza miradi ya maedeleo nchini.

“Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa sekta ya kilimo na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi,” amesema Dkt. Mpango.

Wahalifu 29 washikiliwa na jeshi la polisi
Mwanajeshi wa JWTZ ahukumiwa kwenda jela