Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi, Mohammed Mpinga, amesema wamefanikiwa kukamata vijana 29, ambao ni tishio kubwa jijini Mbeya kwa uhalifu na unyang’anyi wa mali za watu.

Amesema vijana hao wanajulikana kwa jina la wakorea weusi ambao wamekamatwa kwa kujihusisha na vitendo vya kiuhaulifu, kupiga, kuua na kuibia watu vifaa mbalimbali.

Mpinga amewatangaza vijana hao mbele ya vyombo vya habari wakiwa ofisini kwake jumamosi ya leo.

Amesema kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa na wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi utakapokamilika.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.

Kwa upande mwingine, Kamanda Mpinga ametoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato.

Simba SC yatangaza viingilio dhidi ya Al Masry
Tanzania yawasilisha ombi Benki ya dunia