Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka unaoishia mwezi Oktoba, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.1 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2020.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja amesema mfumuko huo wa bei wa Taifa umechangiwa na kupungua na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kinachoishia Oktoba,2020 zikilinganishwa na bei za Oktoba 2020.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua kwa mwezi Oktoba,2020 zikilinganishwa na bei za Oktoba 2019 ni pamoja na mchele kwa asilimia 4.2, Mahindi kwa asilimia 12.4, na unga wa mahindi asilimia 3.2,” amesema Minja

Mbali na hayo Minja alieleza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.4 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba,2020.

Milionea wa Zimbabwe kuzikwa na gunia la fedha
UN yaitaka Msumbiji kuchunguza chanzo mauaji ya kikatili