Burundi iliadhimisha miaka 60 ya uhuru wake mjini Bujumbura kwa gwaride la kijeshi huku nchi hiyo ikiyatupia lawama Mataifa ya Ulaya kwa kuwakumbatia wachonganishi.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye ameipongeza Burundi mpya wakati wa hafla hiyo, akisema baada ya miaka 6 ya kutetea zaidi kesho bora kwa nchi hiyo ya Afrika ya kati sasa mambo yanazidi kuwa shwari.

“Baada ya miaka 60 Burundi haipo kama zamani tena ni Burundi mpya na hii imetokana na kujituma na upendo wa Taifa hili hivyo ni lazima tuienzi sura tuliyoianza, tusikengeuke katika njia nzuri tuliyopita,” amesema Rais Ndayishimiye.

Amesema, “Ukoloni huu ulitugawanya, na hii ilikuwa na madhara mengi. Warundi waliuana wenyewe kwa wenyewe, viongozi wa Burundi hawakuelewa watu wa Burundi ni nani na walipanga mauaji wenyewe”.

Katika Sherehe hizo ambazo pia zimehudhuriwa na Marais kutoka mataifa mbalimbali, Ndayishimiye aliendelea kuonya watu wanaoeneza ukosefu wa utulivu dhidi ya Taifa la Burundi hasa nchi za magharibi zinazoendelea kuwahifadhi watu kama hao.

“Watu wanaovuruga nchi zetu hawapaswi kukaribishwa katika nchi hizi za Magharibi. Maadamu watu hawa wana nchi ambazo wanaweza kutulia na kuishi kwa amani, wataendelea kuzivuruga nchi za Kiafrika. Hivyo basi, iwapo jumuiya ya kimataifa inataka amani nchini Afrika, tunawaomba wasimkaribishe katika ardhi yao mtu yeyote anayesumbua nchi za Afrika,” amesema.

Evarist Ndayishimiye alichaguliwa Mei akimrithi Hayati Rais Pierre Nkurunziza, ambaye kusisitiza kwake kugombea muhula wa tatu madarakani mwaka 2015 kuliiingiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kisiasa na wa muda mrefu ulioadhimishwa na kunyongwa kwa muhtasari, kutoweka, kukamatwa kiholela na kuteswa kwa wapinzani.

Kiwira-Kabulo mbioni kuanza uzalishaji makaa ya mawe
Msomera 'wachekelea' mawasiliano