Ndege ya kivita ya jeshi la Urusi aina ya Su-27 imezua taharuki baada ya kuisogelea kwa karibu ndege ya kivita ya Marekani.

Kwa mujibu wa CNN na Fox, rubani wa ndege ya kivita ya Marekani aina ya P-8 amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiruka usawa wa bahari ndogo ya Baltic lakini rubani wa ndege ya kijeshi ya Urusi alionekana kufanya tukio lisilo la weledi.

Ndege hiyo imedaiwa kuwa ilisogea umbali wa futi 20 karibu na ndege ya Marekani, lakini rubani huyo wa Marekani amedai hakukuwa na hisia za tishio la usalama.

Hata hivyo, msemaji wa kikosi maalum cha jeshi la Marekani, Luteni Kamanda Zach Harrell alikataa kutoa taarifa za kina kuhusu tukio hilo akidai kanuni za kijeshi haziruhusu.

“Kutokana na sera, haturuhusiwi taarifa za usalama wa anga kwa namna hiyo. Kama kutakuwa na tishio la kiusalama katika hali iliyojitokeza tutawapa taarifa zaidi siku za usoni,” alisema Luteni Kamanda Harrell.

Urusi imekuwa imekuwa ikieleza kutofurahishwa na jinsi ambavyo ndege za kijeshi za Marekani zinavyoruka juu ya anga la nchi hiyo pamoja na babari ndogo ya Baltic .

 

 

Taharuki kati ya Marekani na Urusi iliongezeka wiki chache zilizopita baada ya Marekani kuishambulia Syria ambayo ni mshirika mkubwa wa Urusi.

Urusi inamsaidia rais Bashar Al-Assad dhidi ya vikosi vinavyoipinga Serikali, lakini Marekani na washirika wake Ufaransa na Uingereza wamekuwa wakiwasaidia waasi hao.

Timu ya Marekani ilishusha makombora 100 mazito nchini Syria kwa kile walichodai ni onyo dhidi ya tuhuma za Syria kutumia silaha za kikemikali dhidi ya waasi na watu wake. Hatua hiyo ililaaniwa vikali na Urusi ambayo ilidai ni uonevu kutoa adhabu kwanza kisha ndio ufanye uchunguzi.

Odinga awapa neno wafuasi wake
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 2, 2018