Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa vurugu zilizotokea kwenye baadhi ya maeneo ambapo uchaguzi mdogo wa Agosti 12 ulifanyika hazihusiani na majukumu ya tume hiyo.

Dkt. Kihamia amesema kuwa vurugu hizo hazikuathiri uchaguzi wala hawahusiki na vurugu hizo kwakuwa zilifanyika nje ya vituo vya kupigia kura hivyo zinabaki kuwa chini ya Jeshi la Polisi kwakuwa ndio wanahusika na ulinzi wa raia na mali zao.

“Tuna wasimamizi kwenye kila kituo, vurugu zile hazihusiani na tume zilikuwa mitaani sio kwenye vituo vya kupigia kura na sio kila kitu tunashughulikia sisi hata kama mgombea akikamatwa anatoa rushwa sio sisi tutakao muwajibisha ni Takukuru,”amesema Dkt. Kihamia

Akizungumzia suala la wagombea kuporwa fomu za kugombea uchaguzi amesema kuwa wao wanahusika na vitu vilivyo ndani ya uwezo wao kimamlaka, endapo mgombea akiporwa kituoni hilo litakuwa chini yao lakini ikitokea kaporwa nyumbani au barabarani hilo sio jukumu lao.

Hata hivyo, Agosti 12, 2018 katika uchaguzi mdogo wa marudio kwa jimbo la Buyungu na kata 77 bara, vurugu ziliibuka katika Kata ya Kaloleni wilayani Arusha, baada ya kundi linalodhaniwa kuwa ni la wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kudaiwa kumshambulia mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Boniface Kimaro.

Japan kutengeneza gari ya kupaa
Ghana yapokwa nafasi ya kuandaa michuano ya mataifa Afrika kwa wanawake