Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amewahasa madereva wa pikipiki na bajaji maarufu kama bodaboda kutengeneza vituo tambuzi vitakavyokuwa na idadi maalum ya madereva ambao watapewa namba kama ilivyo kwa madereva tax.

DC Ludigija ameyasema hayo alipokutana na madereva hao kujadiliana changamoto zinazowakabili.

Amesema kwa kuwa na vituo tambuzi itasaidia kupunguza uhalifu unaofanywa na baadhi ya madereva bodaboda.

Hata hivyo amewaagiza uongozi wa Halmashauri wa Ilala kushirikiana na uongozi wa bodaboda, TARURA, na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakamilishi ujenzi wa vituo hivyo, huku akiwahasa kuheshimu vituo hivyo pindi vitakavyo kamilika.

Naye Kamanda wa Polisi Usalama barabarani Abdil Issango amewahasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani kwa kuvaa kofia ngumu, kuepuka kupakia mishikaki na kuhakikisha abiria pia anavaa kofia ngumu wakati wa safari ili kupunguza ajali za barabarani

Kamanda Issango amesema jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua madereva na abiria wote watakaovunja sheria ikiwemo kupakia mishikaki na kutovaa kofia ngumu

Kwa upande wao madereva hao wameishukuru kampuni ya 22Bet kwa kuwasaidia vitendea kazi mbalimbali ikiwemo sare za kufanyia kazi na kuitaka serikali iendelee kuwawekea mazingira mazuri ya kazi na kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili.

Watoto 113 wakamatwa kwa uhalifu
Ujerumani yaanza mpango wa kuunda serikali mpya