Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imeanza kwa kupata matokeo ya sare ya bila kufungana katika harakati za kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika nchini Niger mwezi Novemba mwaka huu, dhidi ya DR Congo katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam jioni ya leo.

Ngorongoro Heroes inayonolewa na kocha Ammy Ninje, italazimika kusaka ushindi ama matokeo ya sare ya magoli katika mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa mjini Kinshasa huko DR Congo mwezi ujao.

Kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje amesema kikosi chake kimeonyesha uwezo mkubwa licha ya kushindwa kufikia lengo la kupata ushidni katika uwanja wa nyumbani.

Ninje amesema tayari ameshaona mapungufu yaliyosababisha matokeo ya sare katika mchezo wa leo na ameahidi kuyafanyia kazi katika siku kadhaa za kujiandaa na mchezo wa mkondo wa pili.

Bavicha: Hakuna mwenye uwezo wa kuifuta Chadema
Video: Bombadier aliyofichua Tundu Lissu yaachiwa, Mbowe atuma ujumbe mzito kutoka Gerezani

Comments

comments