Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata wasanii wanne wa kundi la Orijino Komedi akiwemo meneja wao, kwa kosa la kuvaa sare za jeshi la Polisi kwenye harusi ya msanii mwenzao, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Kanda hiyo, Hezron Gyimbi amesema kuwa wasanii hao walikamatwa juzi majira ya saa kumi za jioni na kuhojiwa.

Kaimu Kamanda huyo alieleza kuwa wasanii hao ambao ni Lucas Lazaro (Joti), Alex John (McRegan)m, Isaya Gidion (Wakuvanga) pamoja na meneja wao Sekioni David (Seki), walikutwa na sare za kawaida za Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na filimbi, shati, kofia, mkanda na vyeo, kinyume cha sheria.

“Tunaendelea kuwachunguza zaidi kama wana vitu vingine vya jeshi la polisi na tunataka kujua kuwa sare hizi wamepata kibali kwa nani na uhalali wa kuwa nazo,” alisema na kuongeza kuwa baada ya kuhojiwa tangu juzi jioni hadi jana dhama zao zilikuwa wazi.

Aliongeza kuwa jeshi hilo linaendelea kumtafuta Emmanuel Mgaya (Masanja) ili kujibu tuhuma dhidi yake.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mwaka 202, ni kosa kwa mtu yeyote asiye mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama, kuvaa sare za majeshi hayo au mavazi yanayoshabihiana na majeshi hayo bila kupata kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tundu Lissu apangua hoja za kumng’oa Bulaya Kortini kwa saa mbili
DC Hapi Katumbua Wakuu Wa Shule Za Msingi 68 Na 22 Za Sekondari Wilaya Ya kinondoni Kwa Kuingiza Wanafunzi Hewa