Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amelaani mataifa yenye nguvu duniani, kwa kutumia mataifa yenye mizozo barani Afrika yaliyo na rasilimali kujinufaisha.

Papa ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa jijini Kinshasa DRC, na kuongeza kuwa, “Matokeo yake, nchi hii, iliyoporwa kwa wingi, haijafaidika vya kutosha kutokana na rasilimali zake nyingi.”

Papa Francis wakati akipokelewa alipowasili nchini DRC. Picha ya Vatican News.

Mbele ya maelfu ya Wakongo na Rais Felix Thisekedi, Papa Francis amekemea tabia hiyo huku akiwa na ratiba ya kuongoza misa, inayotarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu jijini Kinshasa.

Aidha, baada ya kuzuru DRC Papa Francis anatarajiwa kuelekea nchini Sudani Kusini siku ya Ijumaa Januari 3, 2023 kuendeleza injili ya upatikanaji wa amani.

Aliyepotea kwa miaka 30 apatikana akiwa hai
Tanzania na Finland zajadili maslahi ya kiuchumi