Mabingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ Simba SC wamewasili salama jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Kigoma, ambapo jana Jumapili (Julai 25) walicheza mchezo wa fainali wa michuano hiyo dhidi ya Young Africans.

Simba SC walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo kutoka nchini Uganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa kutoka Msumbiji, Jose Luis Miquissone.

Simba SC walianza safari majira ya saa mbili asubuhi mkoani Kigoma na kuwasili Dar es salaam saa tano, huku mashabiki na wanachama wakijitokeza Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwalaki.

Kiwango cha watumiaji wa bangi chaongezeka
Biashara United Mara yampigia hesabu Nchimbi